Dalili za kisukari
Dalili za kisukari
Kisukari ni hali ambapo kiwango cha sukari kwenye damu kinakuwa juu kwa muda mrefu. Watu wengi wenye kisukari aina ya 2 hawaoni dalili kwa miaka kadhaa, kwa hiyo kipimo cha damu ndiyo njia pekee ya kujua.
- Kiu kali isiyoisha
- Kukojoa mara kwa mara, hasa usiku
- Njaa ya mara kwa mara
- Kupungua uzito bila kujaribu
- Uchovu au kukosa nguvu
- Kuona ukungu (macho kufifia)
- Vidonda au michubuko inayochelewa kupona
- Maambukizi ya mara kwa mara, kama fangasi sehemu za siri au kwenye ngozi
- Ganzi au kuwashwa kwenye mikono au miguu
Hatari ni kubwa zaidi kwa walio na uzito mkubwa, historia ya kisukari katika familia, shinikizo la damu, umri wa zaidi ya miaka 40, au waliowahi kupata kisukari wakati wa ujauzito.
Nenda hospitali mara moja ukiona:
- Kutapika mara kwa mara au maumivu ya tumbo pamoja na kiu kali
- Kupumua kwa haraka au kwa kina, au pumzi yenye harufu kama ya matunda
- Kuchanganyikiwa, kusinzia sana au kupoteza fahamu
- Kwa anayetumia dawa za kisukari: kutetemeka, kutokwa na jasho, kizunguzungu au kuzimia (sukari kushuka sana)
Nini cha kufanya
- Ukiona dalili hizi, pima sukari ya damu katika kituo cha afya.
- Usianze, usibadilishe wala usiache dawa bila ushauri wa mhudumu wa afya.
- Ukishapimwa, Afya360 inaweza kukukumbusha dawa na kufuatilia vipimo vyako.
Mwongozo huu ni wa elimu tu, si utambuzi wa ugonjwa.
Diabetes symptoms
Diabetes means your blood sugar stays too high over time. Many people with type 2 diabetes have no symptoms for years, so a blood test is the only way to know.
- Constant, strong thirst
- Peeing often, especially at night
- Feeling hungry often
- Losing weight without trying
- Tiredness or low energy
- Blurred vision
- Cuts or wounds that heal slowly
- Repeated infections, such as genital thrush or skin infections
- Numbness or tingling in the hands or feet
Risk is higher if you are overweight, have family members with diabetes, have high blood pressure, are over 40, or had diabetes during a pregnancy.
Go to hospital immediately if you have:
- Repeated vomiting or stomach pain together with strong thirst
- Fast or deep breathing, or breath that smells fruity
- Confusion, extreme sleepiness or passing out
- If you take diabetes medicine: shaking, sweating, dizziness or fainting (very low sugar)
What to do
- If you notice these symptoms, get a blood sugar test at a health facility.
- Don't start, change or stop medicines without advice from a health worker.
- Once tested, Afya360 can remind you about medicines and track your readings.
This guide is for education only and is not a diagnosis.
Vyanzo / Sources
Imekaguliwa / Reviewed: 2026-10-20
Dalili za kisukari · Dalili za UTI (maambukizi ya njia ya mkojo) · Dalili za mimba za mwanzo · Dalili za malaria · Hospitali na kliniki
Privacy Policy
·
Terms of Service
·
Data Deletion
·
Hospitals
·
Dalili / Symptom guides